Taasisi ya tiba ya Mifupa na Upasuaji
wa Mishipa ya Fahamu - MOI, imesema tathmini ya madaktari juu ya afya ya Sheikh
Ponda Issa Ponda inaonyesha amepata mvunjiko bila mifupa kupishana katika mfupa
mkubwa wa bega la mkono wa kulia.
Sheikh
Ponda Issa Ponda.
Kwa mujibu wa taarifa ya kitabibu ya
MOI iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imekuwa vigumu kujua kama jeraha hilo
lilisababishwa na kitu gani na kwamba licha ya tiba ya mwanzo aliyokuwa
amefanyiwa ya kushonwa iliamuliwa afanyiwe upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi
kama kidonda kingeachwa hivyo hivyo, na kwamba bado anaendelea na matibabu.
Kutokana na tukio hilo la kujeruhiwa
kwa Sheikh Ponda Issa Ponda, asasi za kiraia kwa kushirikiana na Mtandao wa
watetezi wa mashirika ya haki za binadamu tanzania unaojumuisha mashirika ya
Tanzania human rights defenders Coalition, kitu cha sheria na haki za binadamu,
SIKIKA, TGNP na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania - TAMWA zimetoa
tamko la kulaani tukio hilo sambamba na kuvitaka vyombo vya dola kuzingatia
misingi ya haki za binadamu na utawala bora wakati wa utekelezaji wa majukumu
yake.
Asasi hizo pia zimeiomba tume ya haki
za binadamu na utawala bora ifuatilie matukio ya matumizi ya nguvu
yanayofanywa na vyombo vya dola katika
sehemu mbalimbali nchini, huku chama cha Sheria Tanganyika, TLS kwa upande wake
kikitoa wito kwa viongozi wa serikali, jeshi la polisi na wananchi kuhusiana na
matumizi ya nguvu kupita kiasi katika ukamataji wa watuhumiwa.
Onesmo Ole Ngurumwa -
Mratibu - Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kwa upande wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam imesema
imemuweka chini ya ulinzi Sheikh Ponda Issa Ponda, kwa usalama wake wakati
akiendelea kupata matibabu na kisha itamkabidhi kwa polisi mkoani Morogoro
ambako jeshi hilo lilieleza kuwa lilikuwa likimtafuta.
Suleiman Kova
Kamishna wa Kanda maalum ya Dar es
salaam Suleiman Kova pia amewaonya wale wote wanaotaka kutumia tukio la
kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda, kufanya vitendo vyovyote
vitakavyoashiria uvunjifu wa amani.
0 comments:
Post a Comment