Advera Senso msemaji wa
jeshi la polisi Tanzania
Kufuatia tukio la
kujeruhiwa kwa kiongozi wa Taasisi za Kiislam nchini Sheikh ponda issa ponda
kuoneka kuchukua sura mpya kadiri wakati na muda unavyozidi kusogea mbele, huku
kukiwa na matamko mbali mbali Hatimaye jeshi la polisi nchini limeweka wazi
kuunda timu yake yenye wajumbe kutoka jukwaa la haki za jina kwaajili ya
kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Mapema leo msemaji wa
jeshi la polisi nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera Senso amesema kwamba
timu hiyo inaongozwa na kamishna wa Polisi Issaya Mngulu tayari imekwishaanza
uchunguzi wa tukio hilo.
Akizungumzia kiini
haswa cha tukio hilo, senso amesema siku ya tukio Piolisi walipanga kumkamata
sheikh pomda kwa tuhuma ambazo amekuwa akikabiliwa nazo kiongozi huyo za kutoa
maneno ya uchochezi sehemu mbali mbali nchini, lakini katika harakati za
kufanya hivyo wafuasi wa kiongozi huyo wa dini waliwazuia polisi kwa kuwarushia
mawe na kasha kufanikiwa kumtorosha mtuhumiwa.
Aidha Tukio hilo
lilitokea iddi pili mjini morogoro baada ya mhadhara uliokuwa ukihutubiwa na
sheikh Ponda issa ponda nakupelekea kujeruhiwa katika sehemu ya begani na kuzua
taharuki za hapa na pale, na sasa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali ya muhimbili kwa matibabu zaidi juu
ya jeraha alilonalo begani ambapo mwenekiti wa CUFalifanikiwa kumjulia hali.
0 comments:
Post a Comment