Kaimu Katibu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw.Moshi Makuka akisisitiza umuhimu wa vilabu kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za mashindano ya SHIMIWI.
Shirikisho la Michezo
ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) linatarajia kufanya mkutano maalum wa
kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu utakaofanyika kesho kutwa
jumamosi ya agosti 31 majira ya saa 4 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa
Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo mtaa wa Luthuli
jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa
SHIMIWI Bw.Moshi Makuka alisema mkutano huo utawahusisha wenyeviti na
makatibu wa vilabu vya michezo ya SHIMIWI kutoka katika Wizara,Idara
Zinazojitegemea,Sekretarieti za Mikoa na Wakala za Serikali.
“Wenyeviti na Makatibu
wa Vilabu vinavyoshiriki michezo ya SHIMIWI mnatakiwa kuhudhuria mkutano huo
bila kukosa ili kufanikisha mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza hivi karibuni”
alisema Bw.Makuka.
Bw.Makuka
aliwataka wenyeviti na makatibu wa vilabu vyote kuja na viambatanisho muhimu
kama vile barua za kuthibitisha kushiriki,fomu za usajili wa wachezaji
watakaoshiriki na vikombe (kwa vilabu vilivyopata vikombe katika mashindano ya
mwaka jana yaliyofanyika mjini Morogoro).
Mashindano ya michezo
ya SHIMIWI kwa mwaka huu yamepangwa kufanyika mjini Dodoma kuanzia Septemba 21
hadi oktoba 5 ambapo yatahusisha michezo ya mpira wa miguu,netiboli,kuvuta
kamba,riadha,baiskeli,karata,bao na drafti.
0 comments:
Post a Comment