Frederick Sumaye - Waziri
Mkuu Mstaafu Tanzania.
Saada Matiku, Mbeya.
Waziri Mkuu mastaafu awamu ya tatu
Fredrick Sumaye amewataka vijana wa vyuo vikuu na mabaraza mbalimbali ya
katiba kutambua na kuchambua kwa kina
mfumo wa Serikali tatu wakati wa
kujadili kwa makini
mchakato wa kupata katiba mpya yenye lengo la kuleta tija kwa watanzania kulingana na mahitaji ya jamii
na kwamba mfumo wa serikali tatu serikali unaweza kusababisha migogoro
zaidi kwa kizazi kijacho.
Ameyasema hayo wakati akifunga
kongamano jumuia ya serikali ya vyuo vikuu nchini TAHILISO katika kujadili rasimu ya katiba mpya lililofanyika
chuo kikuu cha mzumbe kampasi ya Mbeya huku akiwaasa wananchi kuwa makini
katika kujadili mfumo wa serikali tatu…
Amesema kutokana na uzoefu wake wa uongozi ni vema kumaliza
changamoto zinazoikabili mfumo huu wa Serikali mbili ndipo lianze wazo la
kuanzisha Serikali tatu huku akititila shaka kutokea kwa ugomvi mkubwa wa
kupigania rasilimali,vyeo, pamoja na garama za uendeshaji endapo kutaundwa mfumo wa Serikali
tatu zinazopiganiwa kuundwa katika mchakato wa rasimu ya kupitisha
katiba mpya.
Kwa upande wa jumuia ya vyuo vikuu nchini
wamesema kwa kuzingatia uzito wanchi
yetu, tunakoelekea na tulikotoka kufuatia historia ya nchi yetu pamoja na hali
ya maendeleo ambapo Taifa linapita katika hali za
utegemezi ambao ni athari kubwa kwa vijana na watoto kwa wakati ujao.
0 comments:
Post a Comment