Alhaj Ali hassan Mwinyi..Rais mstaafu..
Rais mstaafu
alhaj Ali hassan mwinyi Amezipongeza taasisi za dini ya kiislam nchini kwa
kuwajenga vijana katika maadili mazuri na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano
huo ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili unasababisha kukuthiri kwa vitendo
viovu nchini.
Alhaji mwinyi
alikuwa akizungumza katika hafla ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur
aan yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini dsm.
Amesema
vitendo vya ujambazi, wizi, uasherati na utumiaji wa madawa ya kulevya
vilivyokithiri katika jamii hasa kwa vijana ni matokeo ya malezi mabaya ya
watoto katika jamii wanazotoka hivyo ili kukabiliana na hali hiyo hakuna budi
hatua za haraka za kuwasimamia na kuwalea vijana katika misingi ya dini
zichukuliwe.
Kwa Upande
wake Sheikh mkuu mkoa wa dsm Alhad Mussa salum amesema wazazi hawana budi
kuchukua jukumu la ulezi huku akisisitiza waislam wenye uwezo kuwasidia katika
ujenzi wa vituo vya usomaji Quraan.
Katika
mashindano hayo Mohamed Abdallah Kutoka Sudan alishika nafasi ya kwanza na
kupata fedha taslim shilingi million tano,pamoja na zawadi mbali mbali, mshindi
wa pili alikuwa Abbass mohamed kutoka Nigeria aliyepata shilingi million 3 huku
nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mtanzania Omar abdallah aliyepata shilingi
millon 2 .
Jumla ya nchi
16 duniani zikiwemo Russia, india, Philipines, Kuwait, Naigeria, Yemen na
Afrika kusini zimeshirikia mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment