Dk. Abdallah Kigoda -Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania.
Waziri wa Viwanda na
Biashara Dk. Abdallah Kigoda amewataka wawekezaji wanaozalisha vifaa vya ujenzi
kuhakikisha ubora wa vifaa hivyo unathibitishwa na shirika la Viwango nchini
TBS ili kuondoa mashaka na athari zinazoweza kujitokeza ikiwa hazirtakidhi
viwango vya ubora.
Dk. Kigoda ametoa kauli
hiyo wakati anazindua kiwanda cha vifaa vya ujenzi aina ya Gypsum kinachoitwa
Sunshine Limited ambacho kimejengwa Kibaha Mkoani Pwani kikimilikiwa na
wawekezaji kutoka China.
Amesema katika miaka ya
karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi dhidi ya ubora wa vifaa vya
ujenzi, hatua ambayo imesababisha baadhi ya majengo kuporomoka na kuhatarisha
maisha ya watu.
Naye Mshauri wa siasa
wa Ubalozi wa China aliyehudhuria uzinduzi huo Bw. Li Xu Hang amesema anaamini
ubora wa bidhaa za ujenzi kwenye kiwanda hicho utakuwa suluhisho la nyumba na
majengo yaliyo imara, mbali ya kiwanda hicho kutoa ajira kwa watanzania.
0 comments:
Post a Comment