Tanzania ni miongoni mwa nchi 21 ambazo ugonjwa
wa upungufu wa kinga mwilini (Ukimwi), upo kwa kiwango cha juu kuliko sehemu
nyingine duniani.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vipimo vya Afya
na Tathmini (IHME) hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Washington nchini
Marekani, umebaini kuwa katika kipindi cha miaka 20 idadi ya vifo vitokanavyo
na VVU/Ukimwi vimeongezeka na kufikia asilimia 21.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na
Afisa Habari wa taasisi hiyo, Jackie Karanja, matokeo ya utafiti huo yatachapishwa
Agosti 21, mwaka huu.
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa, mwaka 2010
ongezeko la ukimwi ni asilimia 21 kutoka asilimia 6.2 ya vifo vyote
vilivyotokea mwaka 1990.
“Ukimwi ni sababu inayoongoza na kuwa mzigo wa
magonjwa katika nchi 21, nchi hizo ni pamoja na Afrika Kusini, ambapo Ukimwi
unachukua nafasi kubwa kuliko sehemu yoyote duniani, Tanzania, Kenya na
Uganda,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa watu wengi
walioathirika na ugonjwa huo nchini ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 49
na kusababisha vifo miongoni mwa watu ambao ni wazalishaji na wenye maamuzi na
michango mikubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hata hivyo, utafiti wa IHME umeonyesha kuwa,
licha ya kupungua kwa vifo kati ya mwaka 2006 na 2010, lakini viliongezeka
katika nchi 98, hivyo mwaka 2012 VVU/UKIMWI uliongezeka na kuwa tishio duniani
na siyo Afrika peke yake na nchi 186 ziliripoti kesi na vifo vilivyotokana na
ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment