Edson Monyo (39).
Mfanyabiashara Edson Monyo (39) amefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na
mashitaka mawili ikiwamo kukutwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Sh.
milioni 68.
Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.
Wakili wa serikali Leonard Challo alidai kuwa
Agosti 4, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere alikamatwa na
askari akiingiza kilo 1,512.69 za dawa za kulevya aina ya
Heroin Hydrochloride zenye thamani ya Sh. 68,069,250.
Katika shtaka la pili
ilidaiwa kuwa siku na tarehe ya tukio la kwanza mshtakiwa alikamatwa na askari
akiingiza nchini dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 34.77
yenye thamani ya Sh.13, 908,000.
Wakili Challo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
bado haujakamilika.
Hata hivyo, Hakimu Riwa alisema mshitakiwa
hatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya
kusikiliza kesi ya dawa zenye thamani zaidi ya Sh. milioni 10.
Aidha, kesi hiyo upelelezi wake utakapokamilika
itasikilizwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Mshitakiwa alikana
shtaka la pili la kukamatwa akiingiza bangi nchini.
0 comments:
Post a Comment