Sauti yake na uwezo mkubwa wa
kuimba nyimbo zinazoshikika kiurahisi, umaarufu wake mwingine mkubwa toka enzi
hizo ni kiuno bila mfupa kwa jinsi alivyokua akicheza nacho.Huu ni uwezo
uliofanya mpaka maneno ya kiuno bila mfupa yakapata umaarufu kupitia yeye.
Siku kadhaa baada ya
kutangaza kurudi kwenye muziki kama zamani, Ray C akiwa ametoka kwenye matibabu
ya matumizi ya dawa za kulevya ameanza kujipanga kupunguza unene alionao
ili awe mwepesi zaidi ya alivyo sasa ili kila kitu kiende kama kilivyokua.
Ray C akipiga story na fans wake
alisema “Mauno ni nyonga si manyama”....hii ni moja ya sababu za msingi sana zilizomfanya Rehema
Chalamila kuingia gym kuanza mazoezi.
0 comments:
Post a Comment