Mazungumzo ya tatu ya kisiasa kati ya mawaziri wa
mambo ya nje wa China na nchi za Afrika yamefanyika jana alasiri katika makao
makuu ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema,
China na Afrika zinatakiwa kushirikiana ili kupatia maendeleo kwa pamoja.
Mawaziri hao wamebadilishana maoni kuhusu ushirikiano
kati ya pande hizo mbili, pia wamepitisha taarifa ya pamoja ya mazungumzo ya
tatu ya kisiasa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa China na Afrika.
Bw. Wang Yi amesema, kutimia kwa ndoto ya China
kunategemea jitihada za wachina, pia kunahitaji uelewa na uungaji mkono kutoka
kwa watu wa nchi mbalimbali duniani.
Amesisitiza kuwa waafrika wapatao bilioni
1 wanafanya juhudi ili kutimiza ndoto ya Afrika ya ustawi na maendeleo.
Bw. Wang amesema, China na Afrika ni za jumuia ya
mustakabali wa pamoja, na zinategemeana sana katika njia ya kupata maendeleo.
Anasema,"Siku zote China ni rafiki wa dhati na mwaminifu
wa Afrika, tutaimarisha ushirikiano kati yetu na marafiki zetu barani Afrika
ili kupatia maendeleo kwa pamoja.
Tutawanufaisha wananchi wetu, lakini pia
tutatoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kutimiza amani ya muda mrefu na
ustawi kwa pamoja."
0 comments:
Post a Comment