Frank Lampard amesema
anajali zaidi kuisaidia England kuifunga Ukraine katika mechi ya kufuzu kombe
la dunia hapo kesho kuliko mechi yake ya
100 atakayoichezea nchi hiyo katika mpambano huo.
Kama atacheza mchezo wa
kesho mjini Kiev,Lampard atakuwa mchezaji wa nane katika historia kuichezea
Three Lions idadi ya mechi hizo.
England inaongoza kundi
la H kwa pamoja na Montenegro lakini ikipoteza dhidi ya Ukraine inayoshika
nafasi ya tatu nyuma kwa pointi moja takuwa imejiweka pabaya kufuzu mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment