Waziri Mkuu mstaafu
Edward Lowassa amewataka wasanii wa muziki wa injili kutunga nyimbo zenye
ujumbe unaoweza kulinda na kudumisha amani,umoja na mshikamano wa Watanzania.
Mheshimiwa Mbunge wa
Monduli, Edward Lowassa akiwaaga wananchi.
Kiongozi huyo ametoa
rai hiyo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa albamu ya Dunia haina huruma ya
mwanamuziki nyota wa muziki huo wa
injili nchini Bahati Bukuku.
Amesema kwamba bila
amani hakuna maendeleo hivyo ni wajibu wa wanamuziki wa injili kusaidia katika
kulinda na kutunza amani ya iliyopo kwani amani ikipotea ni vigumu kuirejesha.
Jennifer Mgendi akihudumu.
Mbali na kusisitiza
amani,waziri mkuu huyo mstaafu pia
ametoa mchango wa milioni 20 kwa ajili kusaidia maendeleo ya muziki wa
injili nchini ambapo amempongeza Bukuku kwa kutunga kibao hicho cha dunia haina
huruma ambacho amesema kinazungumzia amani.
MC wa shughuli, Silas
Mbise akishuhudia mgeni rasmi anavyopungiwa
0 comments:
Post a Comment