Timu ya soka ya
Tanzania (Taifa Stars) leo wamerejea nchini wakitokea Gambia walikokuwa
wakicheza mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia
zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Akizungumza mara baada
ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere Jijini Dar
es Salaam,Kocha mkuu wa Stars Kim Poulsen amesema kwamba kufungwa kwa mabao 2-0
dhidi ya Gambia kunatokana na kukosekana kwa wachezaji tisa muhimu wakiwemo
wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Amesema ili timu hiyo
iweze kufanya vizuri kwenye michuano ijayo ni lazima kuwajumisha wachezaji wa
kulipwa ambao mchango wao kwa Stars unahitajika zaidi huku akiwaomba mashabiki
kuendelea kuinga mkono timu hiyo ndani na nje ya uwanja.
Amesema kwamba Gambia
wameshinda mchezo huo uliofanyika Jumamosi iliyopita kwa kuwa iliwaita nyota
wake 12 wanaocheza soka la kulipwa nje ya taifa hilo.
Nahodha wa Stars Juma
Kaseja amewataka mashabiki wawe wavumilivu wakati timu hiyo ikiendelea
kujipanga upya kwa ajili ya michuano ijayo.
Baadhi ya mashabiki,wamesikitishwa na timu hiyo kucheza chini ya kiwango na kuwataka wachezaji kujituma uwanjani huku wakitambua kwamba mpira ni ajira.
Taifa Stars iliondoka
Gambia jana ambapo imepitia Senegal na mali na kisha Nairobi kabla ya kutua
nchini kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya ( Kenya Airways)
0 comments:
Post a Comment