Uongozi
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) umesema unatafakari kwa kina ni
hatua gani watamchukulia naibu spika wa bunge Mh Job Ndugai kwa kitendo cha
kuamrisha askari wa bunge kumtoa nje ya ukumbi wa bunge kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe kwamba hatua hiyo ni ukiukwaji wa kanuni za
bunge zilizo wazi.
Mkurugenzi
wa habari na mawasiliano wa chama hicho Mh John Mnyika ameyasama hayo
alipokutana wa vyombo vya habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho
jijini Dar es salaam na kusema bado wahajajua ni hatua gani watachukua mara
baada ya kukamilika kwa mfululizo wa mikutano ya sekretarieti ya chama
inayoanza kesho chini ya katibu wa chama hicho Dk. Wilbroad Slaa.
Kuhusu
uamuzi wa wabunge wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa lengo la
kutoshiriki kuchangia hoja muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya Mh
Mnyika amesema hakubaliani na vipengele ambavyo vinakataka kutoa fursa ya
kuongeza idadi ya wawakilishi kuongezwa katika muswaada huo ili kutoa haki ya
ushiriki kwa makundi mengi zaidi katika jamii na kupata katiba bora tofauti na
ilivyo sasa, hivyo chama hicho kimesema kitachukua hatua ya kurudi kwa wananchi
ili kuwaeleza upungufu uliopo katika muswaada huo ambao
tayari wabunge wamekwisha upitisha na kusubiriwa kuwa sheria baada ya rais
kuusaini.
Wakati
huo huo Chama cha wananchi (CUF) kimelaani kitendo cha naibu spika Mh Job
Ndugai kuamuru askari wamtoe nje kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe kitendo walichokiita kuwa
ni cha aibu na hakikupaswa kufanya na kiongozi mkubwa
kama huyo.
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Mh Profesa Ibrahim
Lipumba wakati akizungumza makao makuu ya chama hicho jijini Dar es
salaam na kusema kuwa ni wazi kuwa kumekuwepo na
upendeleo mkubwa bungeni baina wabunge wa upinzani na wale wa chama
tawala.
Aidha kuhusu mchakato wa katiba
mpya Profesa Lipumba amesema kuna njama za wazi wazi
ambazo zimekuwa zikifanywa ili katiba mpya iwe ya manufaa kwa
kundio moja na siyo kwa taifa zima.
0 comments:
Post a Comment