Serikali imefanikiwa kununua mtambo mkubwa wa kuchunguza
magonjwa makubwa ya moyo utakaotumika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
kusaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nchi za nje kwa matibabu.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam hapo jijini Dar es
salaam na Mkurugenzi Mtendaji Dk.Marina
Njelekela wakati wa utambulisho wa mtambo huo uliofanyika hospitalinihapo
ambapo amesema mtambo huo utaanza kufanya kazi rasmi
mapema mwezi ujao.
Hata hivyo Dk. Njelekela amebainisha kuwa serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa
wagonjwa waliokuwa wanaenda kutibiwa nje ya nchi na kutoa wito kwa kampuni zote
za bima ya afya nchini kuwalipia wateja wao wanaohitaji huduma mbalimbali za
moyo kutokana na gharama zake kuwa juu.
Aidhakwa upande wake mkuu wa idara ya magonjwa ya upasuaji wa
moyo na utabibu hospitali ya muhimbili Dkt.Robert Mvungi amesema pamoja
na upatikanaji wa mtambo huo bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalamu ambapo amebaini kuwepo kwa madaktari
121 tu kati ya 365 wanaohitajika.
0 comments:
Post a Comment