Zaidi ya wanafunzi laki nane sitini na nane elfu na
thelathini wanatarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi nchini kati
yao wavulana laki nne kumi na mbili elfu mia moja na tano na wasichana ni laki
nne hamsini na tano elfu mia tisa na ishirini na tano
Akizungumza jijini Dar es salaam naibu waziri wa elimu na
mafunzo ya ufundi Mh.Philipo Mulugo amesema mitihani hiyo itafanyika tarehe 11
na 12 mwezi huu.
Mulugo amebainisha kuwa wanafunzi 844,810 wanatarajia kufanya mihihani
hiyo kwa lugha ya kiswahili, 22,535 wanatarajia kufanya kwa lugha ya
kiingereza,na wanafunzi 88 wasioona pamoja na watahiniwa wenye uono hafifu 597
watafanya mitihani hiyo.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa amebaini udanganyifu wa mitihani
umepungua kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kipindi cha mwaka jana.
Hata hivyo ametoa wito kwa
walimu,wanafunzi na wasimamizi wa mitihani hiyo kujiepusha na vitendo vya
udanganyifu kwani serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wote
watakaobainika kukiuka taratibu za mitihani huo na kwenda kinyume na matakwa yaliyo wekwa.
0 comments:
Post a Comment