Kampuni ya Toyota kutoka Japan ndiyo itakayo jenga
bomba la kusafirishia mafuta kutoka Sudan Kusini hadi pwani ya Kenya.
Hii ni kulingana na habari kutoka katika shirika la
habari la Sudan Kusini na mradi huo utagharimu dola za kimarekani bilioni tano.
Nchi ya Sudan Kusini itashirikiana na nchi za Kenya,
Uganda na kampuni ya Toyota kuunda na kudumisha huduma za bomba hilo.
Bomba hili litatoka nchini Sudan Kusini na kupitia
Uganda na kisha kuingia Kenya hadi bandari ya Lamu na kutumika kusafirishia
mafuta ya Sudan Kusini badala ya Kutumia Sudan.
Pia kampuni hii itajenga bomba lingine kutoka
magharibi mwa Uganda ili kutumika wakati Uganda itaanza uchimbaji wa mafuta
yake baadaye mwaka wa 2017.
0 comments:
Post a Comment