Kongamano la kuhimiza maendeleo ya maisha ya watu wa
China na Afrika lilifanyika Beijing.
Wajumbe wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya China na
Afrika walihudhuria mkutano huo.
Afrika ni moja ya kanda zinazoendelea kwa kasi zaidi
duniani, na maendeleo ya kasi yanahitaji uungaji mkono wa uzoefu, teknolojia,
fedha na wataalamu, ndiyo maana Afrika imekuwa soko muhimu na eneo la uwekezaji
kwa China.
Katibu wa shirikisho la China la kuhimiza mawasiliano
ya kimataifa ambaye pia ni meneja mkuu wa kampuni ya kutengeneza mashine nzito
cha China Bw. Lu Wenjun alisema, kuboresha miundombinu na kuinua kiwango cha
maendeleo ya kilimo ni mambo muhimu kwa maendeleo ya Afrika. Akisema:
"kampuni yetu ilishiriki kwenye ujenzi wa miundo
mbinu ya utoaji maji, utoaji umeme, nishati ya viumbe na utengenezaji wa mazao
ya kilimo katika nchi nyingi za Afrika zikiwemo Guinea, Sudan ya kusini,
Ethiopia, Afrika Kusini, Nigeria na Kenya. Naamini kuwa miradi hiyo itahimiza kidhahiri
maendeleo ya uchumi wa Afrika na kuboresha maisha ya watu wa huko, nina hakika
kampuni yetu inakaribishwa kwa dhati na watu wa Afrika."
Zaidi ya miaka kumi iliyopita, ushirikiano ulio chini
ya utaratibu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika pia umepata
maendeleo makubwa.
Ushirikiano huo umeisaidia Afrika ikuze huduma za
jamii na kuinua uwezo wake wa kujiendeleza, na kuboresha maisha ya watu wa
huko.
Kuboresha huduma za matibabu ni moja ya maeneo muhimu
kwa Afrika kutimiza lengo la maendeleo ya milenia la Umoja wa Mataifa, na pia
ni muhimu kwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika kuboresha
maisha ya watu.
Kuzidisha maelewano na urafiki kati ya watu wa China
na Afrika ni jambo muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya
pande hizo mbili.
Katika upande huo, mashirika yasiyo ya kiserikali
yanatoa michango mikubwa.
Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa Tanzania
waliosoma nchini China Fred Maiga alisema:
Mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa China na
Afrika ni msingi muhimu wa uhusiano mpya wa wenzi wa kimkakati kati ya China na
Afrika.
Mwenyekiti wa
shirikisho la Africacare la Kenya Jojo Pio alisema, anatarajia kuimarisha zaidi
ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali ya China.
"China na Kenya zimeshirikiana katika maeneo
mengi, rais wa Kenya alipofanya ziara nchini China alisaini makubaliano mengi
na China kuhusu ushirikiano katika sekta mbalimbali, Tukiwa wajumbe wa
mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kenya, lengo letu ni kushirikiana na mashirika
yasiyo ya kiserikali ya China na kuzisaidia serikali zitimize maendeleo ya
ushirikiano katika sekta mbalimbali."
0 comments:
Post a Comment