Mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Rwanda imetangaza
kuwa inatarajia sekta hiyo kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi nchini
humo.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hio Daktari Richard
Masozera akiongea na gazeti moja la kila siku nchini humo amesema sekta hiyo
inakua kwa haraka jinsi ilivyokusudiwa.
Masozera anaeleza kuwa ukuaji wa sekta hiyo lazima
utachochea kuboreka kwa uchumi sambamba na sekta zingine muhimu za kibiashara
nchini.
Mamlaka hio inaeleza kuongezeka kwa idadi ya abiria na
pia mashirika yanayotumia viwanja vya ndege nchini humo ni ishara ya mamlaka
hiyo inachangia kukua kwa uchumi nchini humo.
Idadi ya abiria wanoatumia anga nchini humo
imeongezeka kutoka 280,000 hadi 500,000 katika muda wa miaka 5 pekee.
0 comments:
Post a Comment