Taasisi ya kibinafsi nchini Tanzania imewataka vijana nchini
humo kujikuza kibiashara ili kuimarisha maisha yao na pia uchumi wa taifa
nzima.
Mwenye kiti wa taasisi hiyo Reginald Mengi akiongea
katika hafla ya kimaendeleo jiji Dar es Salaam amesema vijana hulalamika kila
wakati kwa kukosa ajira lakini wana fursa za kibishara.
Amesema vijana ndio wanaoweza kujikomboa kutoka
katika mtego wa kukosa mapato.
Mengi ameeeleza kuwa kuna fursa nyingi sana za kiuchumi
na kibiashara kwa vijana ikiwa tu watatumia elimu yao na pia ubunifu
kujistawisha kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment