Jason
Nyakundi.
Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa
limejulishwa kwamba Tume ya kimataifa ya uchunguzi dhidi ya Syria inafanya
uchunguzi wake huru kubaini nani anahusika na shambulio la kemikali la tarehe
21 Agosti 2013 kwenye viunga vya mji mkuu Damascus.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Sérgio Pinheiro ameeleza hayo
pamoja na kile ambacho wamebaini kuhusu madhila yanayokumba wananchi wa Syria.
Akihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva
mwenyekiti wa tume hiyo Sergio Pinheiro amesema kuwa matumizi ya silaha za
kemikali ni uhalifu wa kivita.
Aidha ameeleza kuwa wananchi wa Syria wanakabiliwa na
mashambulizi ya mabomu kutoka kwa vikosi vya serikali huku wanamgambo
wakiyalenga maeneo wanayoishi raia ya kaskazini.
Inaelezwa kuwa Miji mingi imebaki kuzingirwa huku
mateso yakiendeshwa kwenye vizuizi vya serikali.
Bwana Pinheiro anasema kuwa vikosi vya serikali
wakiwemo wanamgambo hawaheeshimu sheria zinazostahili kufuatwa wakati wa vita
zinazozuia kushambuliwa kwa maeneo walioko raia kama vile hospitali.
0 comments:
Post a Comment