Kampeni hiyo
inalenga watoto Milioni Moja wa shule za msingi walioathiriwa na mzozo nchini
mwao.
Huku mwaka mpya wa masomo ukianza nchini Syria watoto
wengi wanakabiliwa na changamoto za kurudi shuleni. Ukiwa ni mwaka wake wa tatu
mzozo ulio nchini Syria umeziacha karibu shule 4000 zikiwa zimeharibiwa au
zikiwa makao kwa wakimbizi wa ndani. Kulingana na UNICEF kampeni hiyo inalenga
kuongeza idadi ya watoto watakaojiunga na masomo ambao hawajapata masomo kwa
kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
UNICEF inasambaza mabegi na vifaa vingine vya masomo
kama kalamu na vitabu vya kuandika kwenye majimbo yote 14 nchini Syria.
Wakati
huo huo UNICEF inatoa vifaa vya masomo 5000 , 3000 vya kuchezea na 800 kwa
watoto wanaoanza masomo. Ufadhili zaidi kwa sasa unahitajika ili kuwazesha
watoto zaidi kuendelea na masomo nchini Syria na ni dola milioni 16 ambazo
zimetolewa hadi sasa kati ya dola milioni 33 zilizoombwa.
0 comments:
Post a Comment