Shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limetoa
taarifa mpya inayoonya kuwa homa ya mafua ya ndege aina ya H7N9 na H5N1 bado ni
tishio duniani na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua tahadhari. FAO imesema
kuna uwezekano virusi hao kujitokeza tena katika kipindi cha msimu wa mafua ya
ndege. George Njogopa na taarifa kamili.
Onyo hilo limetolewa wakati Afisa Mwandamizi wa Mkuu
FAO Juan Lubroth alipokuwa na mkutano wa pamoja na maafisa wa shirika la
misaada la Marekani USAID), shirika la Afya Ulimwenguni WHO na shirika
linalohusika na afya za wanyama OIE.
Ili kukabiliana na tatizo hilo la virusi vya mafua ya
ndege, FAO imesema kuwa iko tayari kutenga kiasi cha dola milioni 2 ikiwa ni
sehemu la nyongeza ya dola milioni 5 zilizotolewa na USAID.
Taarifa hiyo pia imeelezea namna dunia ilivyokuwa
tayari kukabiliana na ugonjwa huo wa mafua ya ndege na imewatolea mwito
wananchi kuanza kuchukua tahadhari za mapema.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mkuu wa kitendo cha
maabara wa FAO mwenye makao yake hukoAustralia, maafisa kutoka China na
Marekani.
0 comments:
Post a Comment