Mkutanoni wa
UNCTAD.
Bodi ya usimamizi ya Kamati ya Biashara na Maendeleo
ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, inakutana kujadili jinsi ya kuzisaidia nchi
zinazoendelea kukabiliana na hali ya wasiwasi ilosababishwa na mdororo wa
kiuchumi.
Mkutano huo wa wiki mbili umeanza 16 Jumatatu kwa
hotuba ya Mkurugenzi Mkuu mpya wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi. Bwana Kituyi ambaye
ni raia wa Kenya, alichukuwa wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa saba wa UNCTAD mnamo
Septemba mosi.
Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa na bodi hiyo ni
jinsi ambavyo UNCTAD inatakiwa kuendeleza mienendo mipya ya ukuaji katika
biashara na maendeleo, ushirikiano wa kiuchumi, mchango wa ununuzi wa kitaifa
na kikanda katika kufikia ukuaji endelevu wa kiuchumi.
Mengine muhimu ni mchango wa mitandao ya kimataifa ya
kuongeza thamani ya bidhaa, maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, juhudi za
kuzisaidia nchi maskini na msaada kwa watu wa Palestina.
0 comments:
Post a Comment