Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky ameeleza kwamba, Ban atatangaza
matokeo ya ripoti hiyo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
hii mda mfupi hadi sasa.
Katika upande mwingine Ufaransa, Uingereza na Marekani
zimekubaliana kupendekeza azimio kali katika Umoja wa Mataifa dhidi ya Syria
iwapo nchi hiyo itashindwa kukabidhi silaha zake za kemikali kama
ilivyoafikiwa.
Nchi hizo tatu wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa zimekubaliana kuzidisha mashinikizo dhidi ya serikali ya Syria ili
iheshimu makubaliano yaliyofikiwa kati ya Russia na Marekani kuhusu silaha zake
za kemikali.
Jumamosi iliyopita Russia na Marekani zilikubaliana
mjini Geneva kwamba hadi katikati ya mwaka ujao wa 2014 maghala ya Syria ya
silaha za kemikali yawe tayari chini ya usimamizi wa kimataifa.
0 comments:
Post a Comment