Wananchi wa Rwanda wameshiriki vema katika uchaguzi wa
Bunge huku kukiwa na matarajio kuwa chama tawala cha RPF kinachoongozwa na Rais
Paul Kagame kitashinda uchaguzi huo.
Kuna vyama vitatu vya kisiasa vinavyopimana nguvu
katika uchaguzi huo, huku viwili kati ya hivyo vikionekana kuwa karibu na chama
tawala cha RPF. Tarifa zinaeleza kuwa baada ya vituo vya kupigia kura
kufunguliwa leo asubuhi kulikuwa na mistari mirefu ya wapiga kura katika mji
mkuu Kigali, huku hali ikionekana kuwa tulivu hata baada ya kutokea milipuko
miwili ya maguruneti mwishoni mwa wiki katika soko la Kigali.
Wanyarandwa milioni 6 wamejiandikisha kupiga kura,
huku watu wengi wakitarajiwa kushiriki kwenye zoezi hilo. Bunge lililopita la
Rwanda lilikuwa bunge pekee duniani lenye wabunge wengi wanawake kuliko
wanaume.
0 comments:
Post a Comment