Ruto jana alielekea
katika mahakama hiyo kwa lengo la kusikiliza tuhuma zinazomkabili za kutenda
jinai dhidi ya binadamu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Hayo yanajiri katika
hali ambayo, jana Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisema kuwa, atalazimika
kusimamisha ushirikiano wake na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iwapo
mahakama hiyo itamtaka yeye na Naibu wake William Ruto kuhudhuria vikao vya
kesi zao katika mahakama hiyo kwa wakati mmoja.
Rais Kenyatta na Naibu
wake William Ruto wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika katika machafuko ya
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1400 waliuawa.
Wiki iliyopita Bunge la
Kenya liliupiga kura ya ndio muswada wa kujiondoa nchi hiyo katika mkataba wa
Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Hata hivyo mahakama ya ICC imesisitiza kwamba,
hatua hiyo haitoathiri mwenendo wa kesi zinazowakabili Uhuru na Ruto katika
mahakama hiyo.
0 comments:
Post a Comment