Shirika la Kuteteta Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, watoto wa maeneo ya migodi nchini Tanzania wanakabiliwa na mazingira magumu.
Ripoti ya shirika hilo inabainisha kwamba, watoto
wamekuwa wakijiingiza kwenye ajira ya uchimbaji madini nchini Tanzania huku
wengi wao wakiathirika kiafya.
Aidha ripoti ya Shirika la Kuteteta Haki za Binadamu
la Human Rights Watch imesema kuwa, kuna vitendo vya dhulma na ukatili wa
kingono unaofanywa dhidi ya watoto hao wanaofanya kazi katika baadhi ya maeneo
ya migodi nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya watoto hao wapo
hatarini kuangukia kwenye matatizo ya kiafya, ikiwamo mtindio wa ubongo
kutokana na kemikali zinazopatikana kwenye machimbo hayo ya madini.
Idadi kubwa ya watoto hao hufanya kazi kwenye
mazingira magumu na wakati mwingine hulazimika kuingia kwenye mapango yaliyopo
chini kwa chini, kwa ajili ya kusaka madini, imebainisha ripoti hiyo ya Human
Rights Watch.
0 comments:
Post a Comment