Askofu Kulola alizaliwa Juni 2, 1928 katika Kijiji cha
Nyahonge wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ameacha mjane, watoto 10, wajukuu 44 na
vitukuu 16.
Alifungua makanisa zaidi ya 4,600
ya EAGT ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo Zambia, Malawi, Rwanda na Jamhuri ya
Kidemokrasia Kongo (DRC).
Lakini cha kushangaza ana nyumba
moja tu tena aliyojengewa na waumini wake.
Ni vigumu kuzungumzia historia ya
vuguvugu la uanzishaji makanisa nchini, pasipo kumtaja Askofu Moses Kulola.
Askofu Kulola anajulikana na
wengi kama mtu aliye na nia ya dhati kutangaza neno la Mungu, kutokana na kile
kinachoonekana wazi kwamba hakujilimbikizia mali kama ambavyo tunaona baadhi ya
watumishi wa Mungu siku hizi wanavyomiliki majumba, benki na hata magari ya
milioni ya shilingi.
Hali halisi.
Kwa namna inavyoonekana nchini,
ni kama kuna kundi kubwa la watumishi wanaohubiri kwa lengo la kushibisha
matumbo yao zaidi; Hawana mpango thabiti wa kusaidia yatima wala maskini,
badala yake waumini ndio wanaonyonywa kwa kutoa zaka na sadaka ambazo baadhi
yake hata matumizi yake yamekuwa yakizua maswali.
Utumishi wa Mungu na mali.
“Hakuna shaka kwamba kama kila
nyumba ya ibada Tanzania ingekuwa na mpango thabiti wa kusaidia watu maskini,
yatima na watu wengine wenye hali ngumu, hali ya maisha ingekuwa nzuri zaidi
kwa wengi.
Lakini wapi, baadhi ya watumishi
wako ‘bize’ kujaza matumbo, wanaendesha magari ya kifahari yenye thamani ya
mamilioni ya shilingi badala ya kutumia fedha hizo kutangaza neno la Mungu au
kusaidia wasiojiweza,” anasema Charles Mtanga, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam.
Mtanga anawashauri viongozi wa
nyumba za ibada kuwa na mkakati wa kusaidia yatima na watu wengine wasio na uwezo,
huku wakiendelea kutangaza neno la Mungu, ili wote waweze kuufurahia ulimwengu.
Utanuzi wa huduma.
Kwa mujibu wa Askofu wa EAGT
Sengerema, Joshua Wawa, Askofu Kulola alizaliwa Juni 2, 1928 katika Kijiji cha
Nyahonge wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ameacha mjane, watoto 10, wajukuu 44 na
vitukuu 16.
Katika uhai wake, Askofu Kulola
alifungua makanisa 4,600 ya EAGT ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo Zambia,
Malawi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) na ameacha wosia kwamba
makanisa yafunguliwe kadiri inavyowezekana.
Hata hivyo, licha ya kuwa na
wingi wote huo wa makanisa, Askofu Kulola anamiliki nyumba moja iliyoko mkoani
Mwanza aliyojengewa na waumini.Askofu Moses Kulola.
Wakati Askofu Kulola akifariki
dunia katika mazingira hayo naye Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere
hakuwa na tabia kujilimbikizia mali.
MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment