Taarifa za kushangaza kwamba bondia maarufu nchini, Mbwana
Matumla amekamatwa na madawa ya kulevya nchini Uswisi mara Hispania sasa ni
kama sinema.
Awali ilidaiwa
kuwa, Mbwana alidakwa nchini Hispania akiwa njiani kuelekea Italia kupeleka
mzigo huo ambao mp
aka sasa
taarifa hizo bado ni kizungumkuti.
Baadaye kwa kupitia vyanzo vyetu toka Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi Tanzania ikadaiwa kuwa, bondia huyo alikamatwa kwenye mpaka wa nchi ya
Ujerumani na Switzerland (Uswisi) akiwa na kilo tatu za ‘unga’ aina ya heroin
wenye thamani ya shilingi 150,000,000 za Kitanzania.
Vyanzo hivyo
vilidai kwamba Matumla alikamatwa na polisi wa Uswisi akiwa ndani ya treni
aliyokuwa akisafiria kutokea Ujerumani.
Taarifa zaidi
zinadai kwamba bondia huyo aliondoka Bongo wiki chache zilizopita kwa usafiri
wa basi hadi jijini Nairobi, Kenya ambako alipanda ndege hadi Addis
Ababa, Ethiopia kisha kuelekea Ujerumani ambako alitumia usafiri wa treni
kwenda Uswisi.
Ili kusikia
zaidi kutoka katika familia yake, gazeti hili lilimtafuta kaka wa Mbwana,
Rashid Matumla kwa njia ya simu ambapo alipopatikana alisema ni zaidi ya wiki
mbili sasa hajamuona mdogo wake huyo na akimpigia simu hapatikani hewani.
“Mbwana
hajatuaga alikokwenda, nilihisi kwamba huenda amekwenda Morogoro katika
machimbo ya madini kwani mara nyingi amekuwa akienda huko.
“Mimi kwa sasa
nazidi kuchanganyikiwa kwani nimekuwa nikipokea taarifa nyingi kutoka kwa watu
kuwa amekamatwa na polisi akiwa na unga huko nchi za nje,” alisema Rashid.
Kamanda wa
Polisi wa Kikosi Maalum cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo alisema ishu hiyo
ipo mezani kwake.
“Ni kweli suala
hilo la Mbwana Matumla lipo mezani kwangu na tayari nimeshawaagiza Polisi wa
Kimataifa (Interpol) kulifuatilia,” alisema Nzowa.
Ukifuatilia
maelezo ya polisi, Kamanda Nzowa na familia kupitia Rashid Matumla, maswali
yanayoelea ni mengi kuliko majibu. Uwazi linaendelea kufuatilia, tega sikio.
0 comments:
Post a Comment