Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imesema kuwa watu 60 wameuwawa katika mapigano kati ya wapiganaji wanaomuunga mkono rais
aliyetimuliwa madar
akani Francois Bozize na waasi wanaoshikilia
madaraka.
Msemaji wa serikali Guy Simplice Kodegue
anasema mapigano hayo yalitokea Jumamosi na Jumapili katika mji wa kaskazini
magharibi wa Bossangoa nyumbani kwa Bw. Bozize.
Umoja wa Mataifa unasema
asilimia 80 ya watu wa mji huo ambao wanakisiwa kuwa 30,000 wamekimbilia
porini na maeneo mengine.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema
wafanyakazi wake wawili ni miongoni mwa waliouawa katika ghasia hizo.
Mapigano
hayo yalikuwa kati ya makundi ya wanamgambo na kundi mseto la
waasi wa Seleka ambao walihitimisha utawala wa miaka 10 wa rais Bozize mwezi
Machi .
Kundi hilo la Seleka linajaribu kufanya mabadiliko ya kisiasa ili
kuandaa uchaguzi mkuu wa kitaifa katika muda wa miezi 18 ijayo.
Kufikia
sasa Umoja wa Mataifa unasema ghasia katika taifa hilo zimesababisha wananchi
wapatao 62,000 kutafuta hifadhi nje ya nchi tangu mwanzo wa mwezi huu wa
Septemba.
Jamhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na msururu wa mapinduzi ya
serikali na maasi tangu ilipopata uhuru wake kutoka Ufaransa mwaka wa
1960.http://www.voaswahili.com
0 comments:
Post a Comment