Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeanza
tena mazungumzo ya kusaka amani na waasi wa M23 hapo jana kufuatia muda
uliokuwa umepangwa na viongozi wa eneo la Maziwa Makuu ya Afrika.
Crispus Kiyoga Waziri wa Ulinzi wa Uganda ambaye ni
msimamizi mkuu wa mazungumza hayo ameeleza kuwa, mazungumzo hayo yanatarajiwa
kuwa na mafanikio makubwa na kwamba yanapaswa kumalizika katika kipindi cha
siku 14.
Wiki iliyopita viongozi wa eneo la Maziwa Makuu Barani
Afrika walitoa makataa ya siku 3 kwa ajili ya kuanza tena mazungumzo hayo kati
ya waasi wa M23 na serikali ya Kinshasa.
Kabla ya kuanza mazungumzo hayo hivi karibuni
kulishuhudiwa mapigano kati ya pande mbili huko mashariki mwa Kongo, ambapo
vikosi vya Kinshasa vilikuwa vikiungwa mkono na kikosi maalum cha Umoja wa
Mataifa.
0 comments:
Post a Comment