Image
Image

IRAN YAUNGA MKONO PENDEKEZO LA RUSSIA.



Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba, Tehran inaunga mkono hatua yoyote itakayozuia uingiliaji wa kijeshi wa nchi za kigeni dhidi ya Syria. 

Akihutubia taifa kupitia televisheni jana usiku, Dakta Rouhani amekaribisha mpango wa Russia wa kutaka silaha za kemikali za Syria ziwe chini ya usimamizi wa kimataifa, na kusema kuwa mpango huo umepunguza hatari ya Marekani kuishambulia Syria.

Aidha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kwamba uingiliaji wa kijeshi wa nchi za kigeni nchini Syria utakuwa na madhara makubwa katika eneo, ambayo yatawakumba kwanza wale ambao watasababisha mashambulizi hayo.    
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment