Ibrahim Boubacar
Keita amesema hayo katika kikao cha kwanza na Baraza la Mawaziri na kusisitiza
kuwa, ni jukumu la serikali kutatua kikamilifu migogoro ya maeneo ya kaskazini
na kuimarisha amani ya muda mrefu chini ya msingi wa kuaminiana makabila
tofauti ya nchi hiyo.
Rais wa Mali Septemba 4 wakati alipoapishwa ili kuanza
kuiongoza nchi hiyo pia alisema kwamba, miongoni mwa masuala yanayopewa
kipaumbele na serikali yake ni kuanzisha mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa.
Wakati huo huo Waziri mpya wa Madini wa Mali amesema
kuwa serikali ya nchi hiyo itaangalia upya makubaliano ya madini na kuanza
kuzungumza tena na mashirika ya kigeni kujadili mikataba ambayo haina maslahi
na taifa.
0 comments:
Post a Comment