Makampuni ya ndani katika sekta ya sukari nchini
Tanzania yanasemekana kuelekea kufilisika iwapo uagizaji wa sukari ya bei nafuu
hautadhibitiwa.
Kampuni ya Tanganyika Plantation imetoa mwito kwa
wizara husika kuzungumza na waziri mkuu ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa
tatizo hilo sugu.
Wadau hao wanadai ukwepaji wa kulipa ushuru ndio
sababu kuu ya uagizaji wa sukari,ambapo wanadai hakuna usawa kati ya sukari
inayozalishwa nchini na ile inayoagizwa kutoka nje.
Afisa Tawala wa kampuni ya Tanganyika Plantation Bw
Jaffari Ally anasema kuwa wazalishaji wa ndani wanalipa ushuru lakini
wanaoagiza hawalipi na ndio maana wanaweza kuuza sukari yao kwa bei ya chini.
Alisema iwapo serikali haitaingilia kati na kudhibiti
uagizaji wa sukari , wazalishaji wa ndani huenda wakalizimika kufunga biashara.
Tanzania sasa ina uwezo wa kuzalisha tani 320,000 za
sukari kwa mwaka ilhali mahitaji ni tani 480,000 kwa ajili ya matumizi ya
nyumbani na viwandani.
Mapungufu haya yalipelekea uhaba wa bidhaa hiyo ambapo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alihimiza uagizaji wa tani 50,000 za bidhaa hiyo kila
mwaka lakini sasa wazalishaji wa ndani wanahofia kufunga biashara iwapo
serikali haitadhibiti uagizaji.
0 comments:
Post a Comment