Maonesho ya Pili ya Bidhaa za chapa maarufu za China
Barani Afrika" yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya China, serikali za
mji wa Shanghai na mikoa ya Jiangsu, Zhejiang na Guangdong yamefunguliwa mjini
Dar es Salaam, Tanzania.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa maonesho, waziri mkuu
wa Tanzania Bw Mizengo Pinda amesema maonesho hayo yanawawezesha watu wa Afrika
wafahamu zaidi bidhaa za China na kuzinunua, ili kuongeza uuzaji wa bidhaa za
China nje ya nchi.
Anasema, "Lengo la kuandaa maonesho hayo ni kupambana
na bidhaa "feki" na kujenga imani ya wateja wa Afrika kwa bidhaa
kutoka China. Maonesho haya ni jukwaa muhimu la kuongeza sifa ya bidhaa za
China mioyoni mwa watu wa Tanzania."
Bw. Pinda anatarajia kuwa makampuni ya China na
Tanzania yataweza kuongeza maelewano na ushirikiano kupitia maonyesho hayo, na
haswa yale ya Afrika yataweza kuingiza teknolojia ya China kupitia fursa hii
ili kuongeza uuzaji wa bidhaa za Afrika zenye ongezeko kubwa la thamani katika
nchi za nje..
Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing ameeleza
kuwa makampuni 200 kutoka mikoa 14 ya China, yakiwemo makampuni 10 ambayo yapo
kwenye orodha ya makampuni 500 bora duniani yanashiriki kwenye maonesho hayo.
Bw. Lu anaona kuwa maonesho hayo yatayapatia makampuni ya China fursa ya
kuongeza uwekezaji barani Afrika.
Anasema, "Maonesho hayo yatazisaidia
sana China na nchi za Afrika kujenga ushirikiano wa kunufaishana na kupata
maendeleo kwa pamoja, pia yatawawezesha wanakampuni wa China waifahamu zaidi
Tanzania ili kufanya uwekezaji nchini humo."
Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa nchi za
Afrika umekuwa ukiendelezwa vizuri.
Kutokana na juhudi za viongozi wa China na
Afrika, ushirikiano kati ya pande hizo mbili unaimarika siku hadi siku, na
biashara kati ya pande hizo pia inaendelezwa kwa kasi.
Mwaka 2012, thamani ya
biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 198.49, na
hili ni ongezeko la asilimia 19.3 kuliko mwaka 2011.
Washiriki wa maonesho hayo
ya bidhaa wengi wanatarajia kutumia mwelekeo mzuri wa ushirikiano kati ya China
na Afrika kupanua soko la Afrika.
Mkuu wa kiwanda cha nguo kutoka Guangzhou Bw.
Tan Bingpei anasema,"hii ni mara yetu ya kwanza kushiriki kwenye maonesho
haya, na lengo letu ni kutumia fursa hii kutafuta mwenzi wa ushirikiano wa
kutusaidia kuanzisha biashara yetu barani Afrika."
Bw. Tan anasema kuwa nguo zao zinawalenga wateja za
Afrika, na zina sifa nzuri na bei nafuu. Katika siku ya kwanza ya maonesho
hayo, nguo zao ziliwavutia wateja wengi kuja na kufanya mazungumzo ya
kibiashara nao.
Yeye ana imani kubwa kuwa bidhaa za China zinaweza kupata soko
kubwa barani Afrika.
Maonesho hayo ya siku nne yamegawanyika katika maeneo
manne, yaani mashine na magari; vyombo vya umeme nyumbani, bidhaa za
elektroniki na zile zinazotumia nishati ya jua; bidhaa za matumizi ya kila siku
na vifaa vya ujenzi, kemikali, matibabu na vinginevyo.
0 comments:
Post a Comment