Sheria ya utalii ya mwaka jana ilifuta bodi zote za
mashirika ya umma ili kutoa fursa kwa ajili ya ushindani katika kuajiriwa.Hata
hivyo mchakato huo ulikwama.
Akizungumza jana,waziri wa utalii nchini Kenya
Bi.Phyllis Kandie alisema hali hii itaendelea hadi sheria ya utalii
itakaporekebishwa.Alisema ni vigumu kwa sheria hiyo kutekelezwa.
Chini ya sheria hiyo Rais anateua Mwenyekiti na Waziri
anateua wanachama watano wa bodi.Majina ya watu hao sita yanafaa kuwasilishwa
bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa.
Kandie alisema hali hii imefanya kuwa vigumu kupata
wanachama wa bodi wazuri,na ndio maana baada ya mazungumzo waliamua
kuirekebisha sheria hiyo.
Aidha Bi Kandie alidokeza kuwa wizara yake
inashauriana na Mkuu wa Sheria kuhusu namna ya kufanya marekebisho hayo.
Kucheleweshwa kuundwa kwa bodi hizo huenda kukaathiri
sekta hiyo kwa sababu hakuwezi kutolewa maamuzi yoyote bila idhini ya bodi.
Mwaka jana utalii uliingiza shilingi bilioni 96, Utalii
umekuwa ukikumbwa na matatizo huku wageni wakipungua kwa 29,000 hadi milioni
1.23.
0 comments:
Post a Comment