Kiwanda hicho chenye thamani ya shilingi bilioni 1.7
kinatarajiwa kuunda magari ya zima moto 2,500,malori,mabasi na magari aina ya
'pick-up' kila mwaka kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.
Mkuu wa kampuni ya Foton Jinyu Wang alisema wanajenga
kiwanda hicho ili kuchukua fursa ya kuondolewa kwa asilimia 25 ya ushuru wa
kuagiza magari kwa yale ambayo yataunganishwa ndani ya nchi.
Mpango wa awali wa kampuni hiyo wa kujenga kiwanda hicho
nchini Kenya mwaka jana ulifutiliwa mbali baada ya kuipatia Kampala
kipaumbele,lakini Bw.Wang amesema Kenya imeonekana kuwa kiunganishi muhimu cha
kanda ya Afrika Mashariki.
Alisema itakuwa rahisi kuihudumia Afrika Mashariki
kutoka Nairobi kuliko Kampala.
Hivi sasa magari ya Foton huagizwa yakiwa yamekamilika
lakini pindi kiwanda hicho kitakapoanza kazi ya kuunganisha magari nchini
Kenya,itakuwa fursa nzuri ya kushusha bei na kuweza kuimarisha ushindani wao
katika soko.
Kiwanda cha Foton kitaweza kuajiri raia wa Kenya
takriban 400 watakaohusika katika kazi mbalimbali kwenye kiwanda hicho.
Kampuni ya Foton inajivunia mafanikio katika kipindi
cha muda mfupi tangu kuanza shughuli zake katika soko la Kenya na hususan
Afrika Mashariki mnamo Aprili mwaka 2011 na ina matawi katika mji wa Nairobi na
Mombasa na vilevile wafanyabiashara wengine waliowapa haki za kuuza bidhaa zao
kama vile Eldoret,Nakuru,Thika,Kisumu na Malindi。
0 comments:
Post a Comment