Image
Image

MAREKANI YACHUKUA HATUA ZA KIUSALAMA KUFUATIA MAADHIMISHO YA MASHAMBULIZI YA KIGAIDI YA SEPTEMBER 11.



Ikulu ya Marekani imetoa taarifa ikisema rais wa Marekani Barack Obama jana alikutana na timu yake ya usalama ili kuthibitisha matayarisho na mambo ya usalama katika mkesha wa maadhimisho ya 12 ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa timu ya usalama ya rais inachukua hatua ili kuzuia shambulizi kama la Septemba 11 na pia kuhakikisha ulinzi wa watu wa Marekani na vituo vyake vya nchi za nje. 

Rais Obama amesisitiza kuwa suala la kuwalinda watu wa Marekani waliopo nchini na nchi za nje ni jukumu la kwanza la uongozi katika suala la usalama wa taifa. 

Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza zaidi kuhusu mkutano huo wa Obama na timu yake ya usalama na hatua gani za kiusalama zitakazochukuliwa ili kuzuia mashambulizi.

Awali vyombo vya habari viliripoti kuwa serikali haijapokea tishio lolote la ugaidi katika maadhimisho haya ya Septemba 11.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment