Uchunguzi unaonyesha kuwa israfu au matumzi mabaya ya
chakula yanaweza kusababisha athari mbaya kwa mazingira na kuibua mabadiliko
yenye kuharibu hali ya hewa.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kilimo na
Chakula Duniani, FAO kwa ushirikiano na Shirika la Mazingira la Umoja wa
Mataifa UNEP.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana Jumatano kwenye makao
makuu ya FAO mjini Roma Italia kwa ushirikiano na makao makuu ya UNEP mjini
Nairobi Kenya inaonyesha kuwa karibu tani bilioni mbili za chakula hutupwa kila
mwaka hali ambayo haiathiri tu uchumi bali pia maliasili ambayo ni tegemeo
kubwa kwa binadamu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo
huko Roma, Mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva amesematheluthi
moja ya chakula kinachozalkishwa hutupwa au hutumika kwa njia
mbaya.
Ripoti hiyo
inaonyesha kuwa chakula kinachozalishwa bila kutumiwa hutumia kiwango
kikubwa zaidi cha maji na huchangia karibu tani bilioni 3.3 za gesi inayochafua
hewa kwenye anga ya dunia.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa watumiaji wa kila siku hususan kwenye
nchi zilizoendelea hutumia vibaya chakula kingi sawia na chakula chote
kinachozalishwa barani Afrika kusini mwa jangwa la sahara.
0 comments:
Post a Comment