Wanamgambo kumi wa kundi la kigaidi la Boko Haram
wameuawa katika oparesheni ya Jeshi la Nigeria katika jimbo la kaskazini
mashariki la Borno.
Katika taarifa, Jeshi la Nigeria limesema kuwa kambi
mbili za magaidi wa Boko Haram zimeharibiwa baada ya mapigano katika eneo la
Konduga Jumanne usiku.
Msemaji wa jeshi Luteni Kanali Sagri Musa amesema
ndege na helikopta za kivita zimetumika katika oparesheni hiyo ambapo bunduki
kadhaa za AK-47 pia zimenaswa.
Karibu watu 3,500 wamepoteza maisha Nigeria tokea
kundi la Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009.
Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka
nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na
Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba
na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.
0 comments:
Post a Comment