Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa
(OCHA) imetangaza kuwa, kati ya Machi hadi Agosti mwaka huu zaidi ya watoto 550
wameachiliwa huru na makundi yenye silaha kwenye mkoa wa Katanga huko kusini
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
OCHA imeeleza kuwa, mapambano ya kuzuia kuwaingiza watoto
jeshini na kuwaondoa katika makundi yanayobeba silaha yamefanikiwa ambapo
watoto zaidi ya 550 wameweka silaha zao chini katika maeneo ya kusini mashariki
mwa Kongo.
Duru za habari kutoka Kinshasa zimeripoti kuwa, vituo vya
hifadhi ya muda vya Lubumbashi, Kalemi na Manunu vinawahifadhi watoto 444 huku
133 tayari wamekwishaungana na familia zao.
0 comments:
Post a Comment