Kikao
hicho kilikuwa kimeitishwa kujadili azimio lililopendekezwa na Ufaransa kuhusu
kadhia ya silaha za kemkali nchini Syria.
Duru za kidiplomasia zinasema
wawakilishi wa Marekani, Ufaransa, China, Russia na Uingereza walikutana
Jumatano katika idara ya ubalozi wa Russia mjini New York.
Imearifiwa kuwa kila
upande umeshikilia msimamo wake na kwamba hakuna mazungumzo yenye maana
yaliyofanyika.
Moscow imependekeza kuwa silaha za kemikali za Syria ziwekwe
chini udhibiti wa kimataifa. Ufaransa, Uingereza na Marekani zimependekeza
azimio ambalo linasema serikali ya Syria ikabidhi silaha za kemikali au
ichukuliwe hatua za kijeshi.
China na Russia zimepinga matumizi ya nguvu za
kijeshi dhidi ya Syria.
Ngoma za vita dhidi ya Syria zilianza Agosti 21 pale
magaidi walio ndani ya Syria wanaopata himaya ya kigeni walipodai kuwa serikali
ilitumia silaha za kemikali nje ya Damascus.
Serikali ya Syria imekanusha
vikali madai hayo na kusema magaidi hayo ndio waliotekeleza hujuma ili
kuchochea mashambulio ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo.
Imebainika kuwa magaidi
walio ndani ya Syria wanapata uungaji mkono wa moja kwa moja kutoka Marekani,
Utawala haramu wa Israel, Qatar, Saudi Arabia na Uturuki.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad
Javad Zarif amesema Iran iliionya kuwa magaidi Syria walikuwa wanamiliki silaha
hatari za kemikali lakini Marekani ilipuuza onyo hilo.
Katika mahojiano na
Press TV , Zarif ameongeza kuwa utumizi wa nguvu za kijeshi dhidi ya Syria ni
kinyume cha sheria za kimataifa na ameitaka Marekani isitishe ngoma za kivita
dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
Amesema Iran kama muathirika wa silaha za
kemikali inapinga na kulaani utumizi wa silaha hizo.
0 comments:
Post a Comment