Baraza la habari Tanzania
MCT limesema ni vyuo viwili tu vya uandishi wa habari nchini vilivyokidhi
vigezo vya kutumia mitaala ya kisasa
yenye ithibati ya baraza la Taifa la Elimu ya ufundi NACTE,inayolenga kutilia
maanani uwezo wa mwanafunzi kwenda kufanya kazi inayotarajiwa.
Akitoa taarifa mbele
ya waandishi wa habari kufuatia matokeo
ya ukaguzi wa pamoja wa hivi karibuni baina ya MCT na NACTE,katibu mtendaji wa
MCT, Kajubi Mukajanga,amesema,lengo la ukaguzi huo lilikuwa kubaini uwezo wa
vyuo hivyo ngazi ya cheti na Diploma
katika kutumia mitaala hiyo kwa kuangalia vigezo vya
vifaa,taaluma,Pedagogia,Miundombinu na uongozi.
Bwana
Mukajanga,amevitaja vyuo hivyo kuwa ni cha A3 Institute of Professional Studies cha Dar Es Salaam na cha Arusha Journalism
Training cha Arusha.
Amesema vyuo vitano
vimepewa hadi Desemba mwaka huu kukamilisha vigezo vinavyotakiwa kufundishia
mitaala hiyo yenye lengo la kuongeza weledi katika taaluma ya habari inayotoa
nafasi kubwa ya kazi za vitendo kwa wanafunzi.
Katika hatua
nyingine,meneja wa udhibiti na viwango wa MCT, Pili Mtambalike amewatoa
wasiwasi,wale wote wenye vyeti vya zamani
kuwa mazungumzo yanaendelea kati ya MCT na NACTE,ili kuvitambua kuvifanyia ulinganisho na kuvitambua vyeti
hivyo.
0 comments:
Post a Comment