JINA la
Tanzania limechafuliwa tena baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa
nchini kukamat
wa ikiwa na tani 30 za dawa za kulevya aina ya bangi zenye
thamani ya Pauni za Uingereza 50 milioni (Sh125 bilioni).
Tukio hilo limetokea miezi miwili
baada ya Watanzania wawili kukamatwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150
na thamani ya Sh6 bilioni kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini.
Habari zilizothibitishwa jana na
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), Abdi Omar zilisema
kwamba meli hiyo ilikamatwa juzi ikiwa na mzigo huo wa bangi.
Alisema baada ya kupokea taarifa
za kukamatwa kwa meli hiyo kutoka kwa Polisi wa Kimataifa (Interpol), ofisi
yake iliwasiliana na wakala wake aliye na ofisi zake Dubai, Falme za Kiarabu,
Kampuni ya Philtex ambayo alisema inafanya kazi ya kusajili meli kwa niaba ya
Serikali na kuthibitisha kuisajili.
Alisema meli hiyo ilisajiliwa
mwaka 2011 kwa kazi ya kubeba mizigo chini ya Kampuni ya Gold Star.
Alisema kutokana na tukio hilo,
Kampuni ya Gold Star imekiuka masharti ya Sheria ya Usajili wa Meli na ile ya
Umoja wa Mataifa zinazozuia meli kubeba dawa za kulevya na kuongeza kwamba
ofisi yake itafanya uchunguzi na kuchukua hatua.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda
wa Polisi Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema naye
amesikia kupitia kwenye mitandao kwamba hajapata taarifa za kina... “Leo ni
Jumapili ni ngumu pia kupata taarifa rasmi kuhusiana na hili.”
“Kesho (leo) tutawasiliana na Polisi
wa Kimataifa (Interpol) ili kufahamu undani wa suala hili. Kuanzia hapo ndipo
tutajua nini kinachoendelea, kama waliokamatwa ni Watanzania au la na hiyo
bangi waliitoa wapi.”
Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray alisema: “Sina taarifa za tukio
hilo, labda tuwasiliane kesho.”
Kama sinema.
Taarifa zilizopatikana jana
kwenye mitandao mbalimbali ya kimataifa zinasema meli hiyo ilinaswa maofisa
Forodha na askari wa doria wa Italia waliokuwa Pwani ya Sicily, Bahari ya
Mediterania.
Msemaji wa Idara ya Ushuru Italia, alisema:
“Meli hiyo ilikamatwa baada ya kupatikana kwa taarifa za kiitelijensia kuwa
imebeba dawa hizo, lakini hatukutarajia kama kungekuwa na mzigo mkubwa kiasi
hicho na hata wahusika kuipiga moto.
MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment