Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania,Upendo
Richard akishirikiana na meneja wa duka jipya la Vodacom lilillopo eneo la
Kimara Stop over jijini Dar es Salaam, Eunice Lulinga (kushoto) kukata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa duka hilo,akishuhudia Katikati ni meneja Uhusiano
wa nje wa kampuni hiyo Salum MwalimIkikadiriwa kuwa na wateja zaidi ya milioni kumi na moja, kampuni ya simu ya
Vodacom imesema itaendelea kuchukua juhudi za makusudi kuweka huduma zake
karibu na wananchi ili kuendana na kasi ya ongezeko la wateja sanjari na
kupanuka kwa miji.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo
anaeshughulikia usimamizi wa maduka ya Vodacom Upendo Richard wakati wa hafla
ya ufunguzi wa duka jipya la Vodacom lilipo eneo la Kimara Stop Over nje kidogo
ya jiji la Dar es salaam.
Upendo amesema kuwa Vodacom imeendelea kushuhudia
ongezeko la kasi la wateja ambao wamekuwa wakiishi maeneo mbalimbali wengi wao
nje ya miji hatua ambayo amesema inaipa kampuni yake changamoto ya kuhakikisha
huduma zake zinapatikana karibu zaidi bila kuathiri ubora.
"Tunafuraha kubwa leo hii kuzindua duka la 69 kwa
nchi nzima likiwa ni la 19 kwa mkoa wa Dar es salaam, Jambo zuri kwa duka hili
ni kwamba lipo nje ya mji na hivyo kuwahakikishia wateja wetu kupata kila
wanachokihitaji karibbu na makazi yao na maeneo ya shughuli zao za kila
siku."
"Miji yetu nayo inapanuka na hatuwezi kuwafanya
wateja wetu kuendelea kutegemea maduka yaliyopoameneo ya katikati ya mji ama karibu na mijini lazima tuwafikishie huduma
mahali walipo hata kama ni nje ya miji ili kuwpaunguzia gharama ya muda na
fedha kwa kusafirei kufuata huduma hizo umbali mrefu."Aliongeza Upendo
Upendo amewataka wakazi wa Kimara na maeneo ya jirani kulitumia duka hilo ili
waweze kuendana na shabaha ya Vodacom ya kuwapunguzia wateja wake gharama huku
akiwahakikishia wateja kuwa ubora wa huduama za Vodacom kwenye duka hilo
unakidhi vigezo vya ubora wa maduka mengine.
"Tunaleta huduma karibu na wananchi ili
kuwapunguzia gharama na kero za kusafiri umbali mrefu nataka niwahakikishe
wateja wetu kwamba ubora wa huduma kwenye duka hili ni sawa na za kwenye maduka
yetu mengine kama la Oysterbay, Mlinai City na Samora hivyo kwani linapokuja
sula la kumhudumia mteja kwetu sisi hakuna tofauti."Alisisitiza Kwa upande
wake Meneja wa duka hilo Eunice Lulinga amesema duka hilo litakuwa likitoa
huduma zote za Vodacom ikiwemo usjili wa nambari, Swim Swap, M-pesa.
"Tunawakaribisha wakazi wa Kimara kulitumia duka
hili kwa mahitaji yao ya Vodacom, tunatambua umuhimu wa huduma bora na kuweka
tabasamu kwenye uso wa mteja wetu muda wote ambao Vodacom inawahudumia wateja
wake."Alisema Eunice. Akizungumzia umuhimu wa duka hilo kwa wateja, Mkazi
wa eneo la Kimara Stop Over ambae pia ni mteja wa Vodacom Mohamed Salim amesema
ni ukombozi mkubwa kwao kwa kuwa awali walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata
huduma hasa kwenye duka la Mlimani City.
"Nikiwa mteja wa Vodacom najisikia furaha kubwa
kuona Vodacom imetujali na kutuletea huduma karibu yetu, tunalipokoea kwa
furaha sana kutokana na ukweli kwamba litatupunguzia gharama amabzo tulikuwa
tukilamika kuingia kwenda hadi Mlimani City."Alisema Salim Salim amesema
anatambua kuwa eneo la Kimara kama yalivyo maeneo mengine ya nchi yana uhitaji
mkubwa wa huduma za Vodacom hasa M-pesa, usajili na huduma za kupatiwa laini
mpya ya simu kutokana na sabbau mbalimbali ikiwemo kupoteza.
Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuongeza mtandao wa
maduka yake hatua ambayo imekuwa ikipongezwa na wananchi na wadau wengine hasa
kutokana na jinsi jamii inavyoitegemea M-pesa katika shughuli mbalimbali za
kijamii na kiibiashara.
CHANZO WAVUTI.
0 comments:
Post a Comment