Ishu hiyo nzito ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo
wawili hao walikuwa chooni humo kwa zaidi ya nusu saa na kuwasababishia
usumbufu watu waliokuwa wakitaka kutumia choo hicho.
KISA KILIPOANZA
Siku hiyo ya tukio, mtu mwenye sauti ya kiume alipiga simu
kwenye chumba cha habari , Mwenge jijini Dar na kupasha juu ya tukio hilo.
Alisema:
Mtoa habari huyo alikwenda mbele zaidi kwa kuwaambiwa
waandishi wetu waliompokelea simu wachukue Bajaj au Bodaboda ili kuwahi.
Sosi huyo kabla ya kukata simu aliweka wazi ramani ya kufika
kwenye choo hicho na kusisitiza kwamba muhimu kuwahi kwa sababu huenda
wanagombana.
Kufuatia msisitizo huo, waandishi wetu makini
waliwasha pikipiki zao, kila mmoja na yake na kushika njia kuelekea eneo la
tukio.
Hata hivyo, kwa kuamini wanaweza kukutana na lolote, waliona
ni vyema kwanza kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge
ambapo walipewa askari wawili kuelekea eneo la tukio.
ENEO LA TUKIO SASA
Timu hiyo iliwasili kwenye eneo la tukio. Mlango wa choo
hicho ulikuwa umefungwa lakini kwa mara moja tu haikuwa rahisi kugundua kama
ulifungwa kwa funguo au kawaida tu.
Afande mmoja alijitolea kugonga mlango wa choo hicho
ili kupima ushirikiano utakaotolewa na wawili hao au mmoja wao.
Sauti iliyoonekana ni ya Kanjibai kutokana na kushindwa
unyoofu wa lugha ya Kiswahili ilisikika ikiuliza:
“Nani wewee… taka nini huku?”
Afande: Sisi ni askari polisi, fungua haraka tunajua mko
wawili humo ndani, fungua.
Kanjibai: Subiri kidogo.
Baada ya dakika kadhaa , mdosi huyo alifungua mlango
na kukutwa akiwa na ‘Shabani’.
WALICHOKUWA WAKIKIFANYA CHOONI
Katika maswali ya harakaharaka nje ya choo hicho kila mmoja
alisema la kwake ambalo aliliamini linaweza kumchomoa kwenye skendo hiyo mbaya.
‘Shabani’ alisema yeye aliingia kwenye choo hicho baada ya
kuitwa na bosi wake huyo ambapo alishindwa kumkatalia kwa kuogopa kupoteza ajira
yake na kama inavyojulikana maisha ya Dar bila kazi ni ngumu kuyamudu.
Alipoulizwa walichokuwa wakikifanya ndani ya choo hicho,
Shabani alibaki akiwatumbulia macho maafande.
Kwa upande wake Kanjibai alipotakiwa kujieleza kisa cha
kuingia chooni na mfanyakazi wake, alisema alimuomba wazame humo ili akamnyoe.
Yaani Kanjibai alitaka kunyolewa.
IKAFIKA ZAMU YA KUPELEKWA KITUONI
Afande mmoja aliamuru wawili hao wapelekwe kituo cha polisi,
lakini kabla ya kuanza safari, mdosi huyo aliingiza mkono kwenye mfuko wa
suruali na kutoa vitu vyake kadhaa na kuwakabidhi wadosi wenzake waliofika
‘kumsaidia’ muda mfupi baada ya kunaswa.
Halafu aliingiza mkono kwenye mfuko mwingine na kutoa mafuta
aina ya KY ambayo mtaani hujulikana sana kwa jina la ‘mlainisho’ lakini askari
alimwambia mafuta hayo yanatakiwa kituoni kwa ajili ya ushahidi hivyo asiwape
nduguze.
Breki ya kwanza ilikuwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi
Mwenge ambapo baada ya mahojiano mafupi walihamishiwa Kituo cha Polisi cha
Kijitonyama ‘Mabatini’ ambapo walihojiwa zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Source: GPL
0 comments:
Post a Comment