Mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni
mke wa mtu, amefanya kitendo cha kinyama baada ya kujifungua msalani na kukiua
kichanga chake.
Tukio hilo limetokea hivi
karibuni maeneo ya Mazizini, Ukonga Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada
ya mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana kukitumbukiza kichanga hicho
chooni.
Kwa mujibu wa chanzo chetu,
mwanamke huyo ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar alidaiwa kunywa dawa kwa ajili ya
kuutoa ujauzito aliokuwa nao wa miezi minane na baada ya kuona hali
imebadilika alitoka nyumbani kwake Moshi Bar na kukimbilia Ukonga Mazizini kwa
ajili ya kutaka msaada kwa mama yake mdogo.
Baada ya kufika kwa mama yake
mdogo aliomba maji kwa ajili ya kwenda chooni, hata hivyo alizunguka nyuma ya
choo kwa ajili ya kujipa msaada wa siri lakini hali ilivyokuwa mbaya zaidi,
aliamua kuingia ndani ya choo hicho na kujifungua kichanga hicho na
kukidumbukiza ndani ya shimo la choo.
mashuhuda wa tukio hilo walisema
kuwa walimuona mwanamke huyo akibebwa kwenda ndani kwa mama yake mdogo
ili aweze kupatiwa msaada zaidi lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwa kuanza
kuvimba mwili kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Waandishi wetu walifanikiwa
kuzungumza na mama mdogo wa mwanamke huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la mama
Athony alikiri binti huyo kukumbwa na mkasa huo wakati yeye akiwa kwenye
shughuli zake.
“Kweli nafahamu, alikuwa ni
mjamzito na alifika nyumbani kwangu saa tano asubuhi, alichokifanya hapa si
kitu cha bahati mbaya ni makusudi,” alisema mama huyo.
Mama Antony alisema kuwa
wakati anarudi nyumbani aliukuta umati wa watu na alipoingia ndani ndipo
alipopewa habari za tukio hilo.
Alipotakiwa kutaja jina la binti
huyo, mama huyo alianza kuangua kilio na kuwafanya waandishi wetu
washindwe kuendelea na mahojiano naye.
Mwakilishi wa mjumbe na shina
namba 34 Ukonga Mazizini, Bi Mtende alisema kuwa tukio hilo limewashangaza
kutokana na mwanamke huyo kwenda kutupa kichanga chooni kwa makusudi.
Bi Mtende alisema kwanza mwanamke
huyo siyo mkazi wa maeneo hayo, hivyo hakuna aliyeweza kumjua kwa jina.
Kikosi cha zimamoto na uokoaji
kilifika katika eneo hilo majira ya saa saba mchana kwa ajili ya kutimiza
wajibu waoKikosi hicho kikiwa kimesheheni
zana za uokoaji kilikuta kichanga hicho kikielea chooni na kwa kutumia
mbinu zao za uokoaji na walifanikiwa kukitoa kichanga hicho kikiwa kikiwa
maiti.
Kamanda wa polisi Mkoa wa
Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minangi alikiri kutokea kwa tukio hilo ambalo
yeye aliliita ni la kikatili na mwanamke huyo amepelekwa katika Hospitali
ya Amana kwa matibabu na mwili wa kichanga hicho kimepelekwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Waandishi wetu walifika katika Hospitali ya
Amana kwa ajili ya kupata mahojiano na mama huyo Jumanne iliyopita, hata hivyo.
Mtanda.com
0 comments:
Post a Comment