Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib
Bilal(kulia), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki
mara baada ya kufungua Kongamano la Katiba Mpya na Nafasi ya Wazenjibara
(Wazanzibari wanaoishi bara) .
TAASI za
kiraia Zanzibar zimesema hazijawahi kushirikishwa katika kuiboresha Muswada wa
sheria ya Mabad
iliko ya Katiba Mpya Tanzania.
Taasisi hizo saba ambazo
zinaongozwa na Baraza la Katiba Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Pr. Abdul
Sharif zilisema Bunge halijawatendea haki kwa kunyimwa fursa ya kutoa maoni
katika sheria hiyo. Waliyasema hayo huko Bwawani Zanzibar walipokuwa
wakizungumza na waandishi wa habari jana.
Katibu wa Zanzibar Youth Forum
Alimasi Mohammed Ali alisema kushirikishwa Serikali ya Mapinduzi haina maana
kwamba na wananchi wameshirikishwa.
“Muswada ule ulipokuja mwanzo,
viongozi wa serikali waliitwa Bwawani na sisi raia wa kawaida tuliitwa katika
skuli ya Haile Salasi kutoa maoni yetu” alisema Ali.
Alisema haoni sababu kwa muswada
huu wa sheria hiyo kupewa fursa serikali peke yake na wao kama raia wakaonekana
kama hawana maana.
“Walijua fika kwamba Wazanzibar
hawawezi kukubali kuwa wachache katika Bunge la Katiba na bara kuwa wengi”
alisema Ali.
Alifananisha na tume ya
mabadiliko ya katiba kwamba ilikwenda kwa wananchi mara mbili tofauti. Kwa nini
kamati ya Katiba na Sheria ishindwe. “Hatukubaliani hata siku moja kwa Bara
wawe na 64% na Zanzibar kubakia na 36% wakati ni nchi mbili sawa katika
Muungano” alieleza Ali.
Mwenyekiti wa Baraza la Katiba
Zanzibar Pr Abdul Sharif alisema kwa mujibu wa sheria ingalikuwa vyema Muswada
huo ukaonekana katika magazeti ili wananchi watoe maoni yao.
“Mimi mwenyewe nilikuwa na
mapendekezo yangu lakini hawakunipatia fursa ya kutoa mawazo yangu” alisema Pr.
Sharif.
Alisema wameutoa mswada huo
katika kabati na kuupeleka Bungeni tu, halafu wanajidai wananchi wamepata fursa
si kweli. Aliendeleaa.
Taasisi ambazo zimeshiriki
mkutano huo ni pamoja na TAMWA, Zanzibar Youth Forum, Zanzibar Law Society,
Baraza la Katiba, Pemba Press Club, Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo
Zanzibar na ZAFELA.
MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment