Image
Image

NCHI 5 ZA EAC ZAIANDIKIA ICC BARUA IMRUHUSU RUTTO AWEZE KUENDELEA NA MAJUKUMU YAKE NCHINI MWAKE.




Nchi 5 za Afrika zimeiandikia barua Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) zikiitaka imruhusu Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kuwakilishwa mahakamani na mawakili wake ili apate fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kikatiba nchini mwake.

Nchi hizo ambazo ni Tanzania, Burundi, Rwanda, Uganda na Eritrea pia zimeitaka ICC kubadilisha kifungu cha 63 cha mkataba wa Roma kinachosisitiza kuweko mahakamani mshukiwa wakati wa kusilikizwa kwa kesi yake. 

Habari za kuminika  za karibu na mahakama hiyo ya kimataifa zinasema Umoja wa Afrika (AU) pia umeandika rasmi barua kama hiyo kuhusiana na kesi ya William Ruto.

Makamu wa Rais wa Kenya alikuwa mjini Hague, kuanzia Jumatatu iliyopita wakati kesi yake ilipoanza kusikizwa Septemba 10. 

Hata hivyo alilazimika kurudi nyumbani siku ya Alhamisi baada ya Mwendesha Mashtaka wa ICC, Bi. Fatou Bensouda kuomba kesi isitishwe kwa muda wa wiki moja ili kumpa nafasi ya kupanga mashahidi.

Nchi za Afrika zimekosoa Mahakama ya ICC kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni ubaguzi wa kisheria. 

Nchi nyingi barani humo zinaamini kwamba ICC inatumiwa kisiasa na nchi za Magharibi ili kufikia malengo fulani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment